Gurudumu la Uchumi

Gurudumu la Uchumi

Fahamu masuala kadha wa kadha kuhusu uchumi kama vile, namna ya kupambana na umaskini, mfumuko wa bei, kushamiri kwa matumizi ya dola na athari za kuyumba kwa uchumi wa dunia kwa nchi za Afrika. Mada hizi zinafanyiwa utafiti wa kina na zinazungumzwa kwa lugha rahisi inayoeleweka ili kukufanya uelewe na usichoke kusikiliza .

00:00
00:00

Episodens resumé

Mwezi uliopita viongozi kutoka Afrika walisafiri hadi Moscow Urusi kwa mkutano uliolenga kuimarisha ushirikiano baina ya bara hilo na Urusi, hata hivyo swali ambalo watu wengi wanajiuliza ni kwanini Afrika ni kama ina iamini sana Urusi? Tumezungumza na Francis Ibrahim, mtaalamu wa masuala ya diplomasia.

Episoder

317-

Mkutano wa Urusi na Afrika, Moscow inatafuta nini kwa bara hili?

Mwezi uliopita viongozi kutoka Afrika walisafiri hadi Moscow Urusi kwa mkutano uliolenga kuimarisha ushirikiano baina ya bara hilo na Urusi, hata hivyo swali ambalo watu wengi wanajiuliza ni kwanini Afrika ni kama ina iamini sana Urusi? Tumezungumza na Francis Ibrahim, mtaalamu wa masuala ya diplomasia.

11 nov. 2026
316-

Gazeti linapogeuzwa kuwa penseli ya kuandikia

Msikilizaji, je, wajua kuwa gazeti la zamani linaweza kugeuzwa kuwa penseli na wakati huo huo kutoa ajira kwa vijana? Huo ndio ubunifu wa wajasiriamali wawili katika eneo la Athi River nchini Kenya ambao wamegeuza magazeti yaliyotumika kuwa fursa ya biashara na chanzo cha kujikimu kimaisha.

04 nov. 2026
315-

DRC: Ufugaji wa nyuki unavyokwamua maisha ya raia wa mji wa Goma

Mji wa Goma, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, unaendelea kukabiliwa na changamoto za kiusalama na kiuchumi, huku ukiwa chini ya udhibiti wa waasi wa FRN wanaoongozwa na rais wa zamani Josephu Kabila, ambako fursa za ajira ni chache na vijana wengi wanakabiliwa na changamoto ya kujipatia kipato, hata hivyo baadhi yao wameamua kutafuta njia mbadala za kujikimu na kusaidia familia zao.

21 okt. 2026
314-

Afrika kuzindua taasisi ya ukadiriaji mikopo, je itasaidia?

Afrika imezindua rasmi Wakala wa Ukadiriaji wa Mikopo wa Afrika, Africa Credit Rating Agency (AfCRA), hatua inayolenga kushughulikia changamoto za gharama kubwa za mikopo na kuvutia uwekezaji zaidi kwa ajili ya maendeleo ya bara hilo. Je, kuanzishwa kwake kutapunguza kweli gharama za mikopo kwa mataifa ya Afrika, au ni mwanzo tu wa safari ndefu ya mageuzi ya kifedha?

14 okt. 2026
313-

Je, Afrika itapata sauti inayodai katika uchumi wa dunia?

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, nchi nyingi za Afrika zinakabiliwa na mzigo mkubwa wa madeni na gharama za juu za kukopa katika masoko ya kimataifa. Fedha nyingi ambazo zingetumika katika afya, elimu, miundombinu na ajira zinaishia katika kuhudumia madeni, hali inayoweka shinikizo zaidi kwa uchumi wa nchi hizi. Je, hitaji la Afrika la kuwa na mfumo mpya wa kifedha duniani wenye uwakilishi na usawa zaidi litawezekana?

07 okt. 2026